MWALIMU ZAWADI NGAILO Cover Image
MWALIMU ZAWADI NGAILO Profile Picture
MWALIMU ZAWADI NGAILO
@mwalimuzawadingailo
4 people like this
0623132195

Uwezo wa kutufanya hai.
“maana mtu hatoishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu” Mathayo 4:4, neno limejaa uwezo wa kutufanya hai, kama vile mwili bila chakula unakufa ndipo mtu aliye na Yesu bila neno lake lazima atakufa kiroho. Neno la Mungu linatupatia nguvu ya kuishi bila neno la Mungu maisha yetu ya kiroho yamo hatarini, Petro akamwambia Yesu “basi twende kwa nani wewe unayo maneno ya uzima” maneno ni uzima!
Uwezo wa ushindi dhidi ya shetani.
“tweni upanga wa roho ambao ni neno la Mungu” Waefeso 6:17b ,. Mkristo asiye na neno la Mungu ni sawa na mwanajeshi asiye na silaha alafu yuko vitani, neno la Mungu ni salaha kuu dhidi ya shetani “je, neno langu si kama moto, asema Bwana, na kama upanga ukatao kuwili?” neno la Mungu ni ushindi mkamilifu dhidi ya shetani! Tukijua kulitumia ni ushindi mkamilifu!
Uwezo wa kupokea kutoka kwa BWANA.
“…….na maneno yangu yakikaa ndani yenu , ombeni lolote mtalipata” Yohana 15:17. Neno likijaa ndani yetu tutajua jinsi ya kuomwomba Mungu sawa sawa. Ni muhimu kuishi kwa kusoma neno la mungu ili tuombe sawa na mapenzi yake .
Uwezo wa kuumba.
“kwa imani twafahamuya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa NENO LA MUNGU….” Waebrania 11:3. “maana yeye alisema ikawa,NA YEYE ALIAMURU IKASIMAMA” Zaburi 33:9 neno lina nguvu ya kuumba inategemea unaamuru nini na kwa uweza gani! Hivyo hata ukipita katika ugonjwa unaweza ukasimama mwenyewe ukaamuru kwa uweza wa kuumba na ugonjwa ukaondoka. Yesu alikuwa anatumia maneno kama haya kuponya watu “nataka takasika” uwe mzima” “mtoke mtu huyu” haya ni maneno ya kuumba kama Mungu alivyo tamka “iwe nuru ikawa n.k.” mwanzo 1:1-.. .
Ni Mungu mwenyewe.
“hapo mwanzo kulikuwa na neno , naye neno alikuwako kwa Mungu naye neno alikuwa Mungu” Yohana 1:1 ,. Neno la Mungu ni Mungu mwenyewe, kwasababu huwezi kumtofautisha mtu na neno lake , Mungu ni neno na ndio maana sisi tukilishika neno lake tunakuwa washiriki wa tabia ya kiungu “…tupate kuwa washiriki wa tabia ya kiMungu…” 2Petro 1:4,. The Amplified Bible says that “ sharer (per-takers) of divine nature” na kwa namna hiyo tunaitwa miungu “mimi nimesema ndinyi miungu,na wana waa aliye juu wote pia..” Zaburi 82:6. Kumbe tunapata uwezo wa kuumba kwasababu na sisi ni mi ungu kwa kulishika neno lake!
Tunapataje uwezo wa Neno la Mungu!
“hapo mwanzo kulikuwa na neno, naye neno alikuwako kwa Mungu naye neno alikuwa Mungu, . Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa yeye; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima , nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo yang’aa gizani wala giza halikuiweza!” Yohana 1:1-5 ,.
Mambo ya kujifunza kutoka kwenye hilo andiko!
1.) Neno la Mungu ni Mungu mwenyewe hivyo si la kulifanyia mzaha, kamwe huwezi kumtenganisha mtu na neno lake , ndiyo maana hata Mafalisayo walimtega Yesu kwenye maneno yake ili wamkamate “wakamviziavizia …ili wamnase kwenye maneno yake, wapate kumtia kwenye enzi ya mamlaka ya liwali” Luka 20:20. Neno la Mungu ni Mungu mwenyewe.
2.) Tunajifunza jinsi ya kulitumia neno la Mungu , biblia inasema “ ndani yake ndimo ulimokuwa uzima” ni muhimu kujua kusikia neno tu haitoshi bali kujua kilichoko ndani ya neno hilo, Neno la Mungu lina uzima ndani yake ambao huwezi kuupata kwa kusikia peke yake! Ni kweli kusikia neno la Mungu kunaleta imani(warumi 10:17) lakini imani inatakiwa kuwekwa kimatendo hapo inamaanisha udhihirisho wa neno ulilolipokea na hapa ndipo wakristo wengi wanashindwa kujua na kubaki kumlaumu MUNGU!

Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake.
Isaya 48 :16

17 Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
Isaya 48 :17.

Asante Yesu maana upo nasi kila wakati nahitaji uwepo wako katika maisha yetu tuongoze na kutusimamia tufike salama.Bariki watu wote wanao litafuta jina lako mchana na usiku.

Tell me, listen to these; from the beginning I have not spoken in secret; since they were, I am; and now the Lord God hath sent me, and his spirit.
Isaiah 48:16

17 This is what the Lord, your Redeemer, the Holy One of Israel, says: I am the Lord your God, teaching you to benefit yourself, leading you in the way you should follow.
Isaiah 48:17. Thank you Jesus that you are always with us and need your presence in our lives to guide us and to secure us securely. Bless all those who search your name day and night.
Maisha na Neno la Mungu Ministry