KUWA MAKINI KESHO KUEPUKA USUMBUFU.


Kesho asubuhi, April 1, 2017 kutakuwa na ule upuuzi wa " Siku ya Wajinga Duniani ", katika taarifa na habari mbalimbali kupitia mitandaoni.

Napenda kuwakumbusha wapendwa wote, kuwa makini na baadhi ya taarifa mbalimbali zitakazokuwa zikitolewa siku ya kesho (hasa asubuhi) kupitia mitandao na sehemu nyingine kuwa, zinaweza kuwaletea sintofahamu au usumbufu kwa muda katika shughuli zao, kama hawatokua makini.

Taarifa zangu za aina yeyote ile siku ya kesho, hazitahusika na upuuzi huo wa 'Siku ya Wajinga', kwa sababu mimi si mmoja wa wafuasi au waamini siku hiyo

Like