#chakushangaza
DUNIA ITASAHAU YALIYOIKUMBA MJI WA ALMERO NCHINI COLOMBIA, LAKINI KAMWE HATUWEZI KUMSAHAU BINTI WA MIAKA 13 OMAYRA SANCHEZ (Inasikitisha mnooo).

Mji wa Almero ulizama ndani ya tope zito la Vilacano muda mchache baada ya mlipuko uliotokea mnamo tarehe 13 Novemba 1985 saa 3:15 usiku. Tahadhari ilitolewa na mamlaka mbali mbali za hali ya hewa kwamba kuna hali ya hatari siku chache zijazo kabla ya janga hili zito kutokea.

Haikuchukua zaidi ya masaa mawili tu baada ya mlipuko huo hatimae mji mzima wa Almero ukawa umezama kwenye tope la Valcano.

Akiwa miongoni mwa watu waliokumbwa na mafuriko haya, Omayra alikuwa msichana wa miaka 13 tu wakati huo. Siku ya tukio Omayra alikuwa na kaka yake pamoja na shangazi yake. Mama yao alikuwa amesafiri kwenda mjini Bogota kibiashara.

Kadhia zote za mtetemo, ngurumo na pilika zingine za kuomboleza walizisikia. Hakukuwa na namna ya kutoka na kukimbia. Uwe nje uwe ndani tope lingekufikia tu. Tayari walishazungukwa na mafuriko na sasa walijikunyata ndani wakisubiri tu kusombwa. Nyoyo zilijaa hofu ya kifo. Ghafla nyumba yao ilipigwa kwa kishindo na kila kitu kutawanyika.

Hekaheka za kujinasua kutoka kwenye tope wakati nyumba ikititia na kuzama zilipamba moto. Kila mtu alipambana kivyake. Baada ya muda kupita, Omayra alijikuta akiwa amenasa kwenye tope ambalo chini yake ndiko nyumba yao ilikotitia na kutawanyika. Alifunikwa hadi shingoni na takataka nyingi mbali na tope lenyewe la Volacano.

Waokoaji waliokuwa wameshaanza kufika eneo la tukio, waliuona mkono wake ukiwa umekamata kipande cha mti mwembamba. Walijaribu kumnasua. Wakamfukua hadi kiunoni, wakaishia hapo. Kwa kuwa haikuwezekana tena kumtoa zaidi. Kila walipomvuta hakutoka. Mbaya zaidi, maji yaliyojitenga na tope yalianza kuja juu. Walihofia angezama.Wakamvalisha tairi ili asizame. Maji yaliendelea kuja juu polepole.

Eneo zima lilijaa vilio vya hofu, maumivu na kuomba msaada. Vifaa vilikuwa duni mno, na waokoaji walikuwa wachache mno kulinganisha na idadi ya watu waliokuwa wakihitaji kuokolewa. helkopta mbili tatu zilizobeba majeruhi hazikutoshea hata kidogo. Ajabu, Omayra alikuwa mwenye matumaini sana. Katikati ya hali ile aliimba, alizungumza na waokoaji, alikubali kuhojiwa na mwandishi wa habari.

Aliomba kupewa maji, biscuit au soda. Alikuwa mwenye matumaini ya kutoka pale. Kwake yeye kuwa mzima baada ya kusombwa na tope lile kulimaanisha uhai. Alitaniana na kucheka na waokoaji waliokuwa wakitafuta namna ya kumtoa.

Muda zaidi ulikatika bila mafanikio, waokoaji waligundua hawawezi kumtoa Omayra pale alipokwama. Ilionekana miguu yake ilikuwa imejikunja huko chini mithili ya mtu aliyepiga magoti. Njia pekee iliyoonekana kufaa ilikuwa kuikata miguu ya Omayra ibakie huko chini na yeye atolewe. Tatizo likawa, wangemkata na nini sasa? Wangemkataje katika hali ile na mazingira yale? Ilikuja kugundulika baadaye huwa marehemu shangazi yake aliyekuwa chini huko akiwa amebanwa na matofali ya nyumba na mbao alikuwa ameikumbatia miguu ya Omayra kwa nguvu mno mno mno. Ndiyo sababu ya Omayra kukwama akiwa amepiga magoti. Taratibu uchangamfu wa Omayra ulianza kupotea. Hofu ya kifo ilianza kumvaa.

Maumivu yalianza kuzama mwilini mwake. Alianza kulia na kusali kwa sauti. Hii iliongeza simanzi zaidi. Waokoaji hawakujua wafanye nini tena kumsaidia. Iliumiza mno kushuhudia kutetereka kwake. Saa zikazidi kuyoyoma Omayra akiwa vile vile, pale pale. Kila walipojaribu kumvuta maji yalikuja juu naye akadidimia kwenda chini zaidi. Mikono yake ikaanza kufa ganzi na kupata rangi nyeupe. Akaanza kuchanganyikiwa na kupayuka. Kuna nyakati aliomba wamtoe kwa kuwa angechelewa shule na kuadhibiwa.

Hali ilipozidi kuwa tete, Siku ya tatu tangia kunasia pale ardhini, rangi ya mwili mzima iligeuka kuwa nyeupe na macho yake yalianza kuvilia damu, wakati huu Omayra aliacha kulia na kutapatapa, alianza kuaga watu akiwemo mama yake ambaye alikuwa mbali na upeo wa macho yake. Ni kama vile maumivu aliyokuwa anayasikia yalikuwa makali mno. Alikuwa ameteseka kwa takribani saa 60! Karibia siku 3 za mateso makali hatimae binti mrembo OMAYRA

Like