Tuungane kutetea haki yetu Mitandao ya simu mnatuibia Mb


Kila anayesoma hii awatumie watu kumi mpaka Watanzania wote wajue haki yao bonyeza share hapo chini kwenye whatsapp, facebook, twitter, telegram mpaka hawa watu watusikie kilio chetu.

 Grabilla screen capture:
Miaka hii ya Teknolojia na mawasiliano nilitegemea gharama za internet / data kuwa chini zaidi, Ila cha kushangaza ISP / Hawa wanaotoa huduma ya internet wanaongeza gharama zaidi wanapoona watu wanatumia data sana.
 
Hii mnakosea sana ISP mlitakiwa kupunguza gharama za internet kadri watu tunavyoongezeka kutumia internet, wekeni faida kiduchu kwenye data wakati huohuo mapato yenu yataongezeka kutokana watumiaji wa data kuwa wengine zaidi.
 
Mikonga ya fiber iko kibao kuna ule Wa SEACOM na ule wa taifa NICTBB Ila cha kushangaza bado data zinapanda tu deile badala zishuke na watu tuko wengi tunaishi kwa internet.
 
Punguzeni gharama za internet kila mtu ana smartphone sasa na pia ili kwenye internet cafe wasiweke matangazo ya kusema huruhusiwi kuchek YouTube au kudownload, maana Mimi nimeenda kuchek YouTube hapo internet badala ya kuweka bando ambao mngefaidi ISP, Ila mkiweka bando afodabo kwa mfano kwa TZS. 500 napata 1GB kwa mwezi basi Wa bongo wote tutahamia mtandao wako.
 
 
Usikose kutuunga mkono kwa kukomenti hapo chini maoni yako kuhusu bei kubwa ya internet. Saidia kufikisha kilio chetu kwa watu wengi waitambue, Viongozi pia mnaosoma makala hii mtusaidie kuwatazama hao watoa huduma mbona kipindi cha kikwete mb zilikuwa bei ndogo hata kaba ya mkongo wa Taifa kuzinduliwa? Hata sielewi hizi bei zinatoka wapi. jamani maisha yetu yanategemea Mb siku hizi mtusaidie kupunguza gharama
 
Kila anayesoma hii awatumie watu zaidi ya kumi mpaka Watanzania wote wajue haki yao bonyeza share hapo chini kwenye whatsapp, facebook, twitter, telegram mpaka hawa watu watusikie kilio chetu. Harakati hizi zimeanzishwa na mdao wa jamiihuru.com