Kutangaza biashara facebook ni kupoteza pesa zako jifunze zaidi hapa


Jifunze wapi utangaze biashara yako na wapi usitangaze kwakua utapoteza pesa zako

Habari ndugu mfuatiliaji wa makala zangu zinazohusu jinsi ya kufanya biashara, Jinsi ya kutangaza biashara mtandaoni na makala nyingine ambazo zinakusaidia kujijenga kibiashara. Nashukuru mtandao wa www.jamiihuru.com unasaidia kutuwezesha vijana kuweza kujiajiri wenyewe badala ya kutegemea ajira za kwenye makampuni ya watu.

Leo nazungumzia sababu kuu mbili ambazo sikushauri kulipia pesa yako kwa lengo la kutangaza biashara yako au blog yako au youtube yako au page yako facebook bora hizo pesa unazolipia facebook ufuge kuku ambao hutahitaji kutangaza bali utawapeleka sokoni na utawaauza.

Facebook ni mtandao wa kigeni unamilikiwa na bwana Mark zuckerberg  aliyopo huko marekani. Chanzo kikuu cha mapato facebook ni matangazo ya kulipiwa. facebook inatengeneza mamilioni ya pesa kupitia matangazo ambayo watumiaji wa facebook wanalipia ili kutangaza huduma zao au biashara zao. 

Nashangaa mtu amefungua page facebook eti anaitangaza humo humo facebook ili ipate likes nyingi akidhani eti ataitumia kwa marketing ni kupoteza pesa na muda wako.

Nimetangaza facebook kwa muda wa miaka 5 Nimetangaza google kwa muda wa miaka 5 Majibu niyopata bora kutangaza google lakini sio facebook

Sababu za msingi ambazo facebook haifai kutangaza biashara ni hizi

Watanzania wengi wanatumia facebook bure yaani bila kulipia internet sasa ukitangaza blog facebook kwa lengo la kupata wasomaji kwenye blog yako andika umepoteza pesa bure. Mtu akibonyeza link ili atembelee blog yako hawezi kwenda kwenye blog yako kwakua hana internet. Yupo facebook bure bila internet 

Sababu nyingine hata ukipromote page ya facebook unapoteza muda watu watalike hata milioni lakini page yako haitakusaidia kuuza chochote kwakua waliopo facebook wengi wana visimu vidogo visivyo na uwezo wa kusoma hata ebooks, Ukitaka kujua zaidi fanya utafiti zaidi.

Sababu nyingine facebook inaonesha tangazo lile lile kwa watu wale wale siku zote sasa mtu alishaona tangazo lako na lililipia lakini kila siku ataendelea kuliona na kulipia hapo unapoteza pesa bure kutangaza kitu kile kile kwa mtu yule yule. 

Je wapi unaweza kutangaza biashara ukawapata watu wapya?

Sina ubia ya google lakini nakushauri Tangaza baishara yako google adwords. Ni kweli ni gharama lakini gharama ni kama facebook tu, Facebook unalipia baada ya kuonesha matangazo yaani ni kama mkopo lakini huduma yao haina matokeo mazuri kwa biashara zako. Google unaweka dola 10 kisha inaanza kupungua kidogo kidogo mpaka iishe kulingana na idadi ya wanaobonyeza matangazo yako.

Ukiwa unatangaza google tumia kuonesha tangazo kwenye search networks tu na sio display network, Seacrh networks ni gharama nafuu kutangaza kwakua pesa yote inaienda kwa kampuni ya google tu wakati ukitangaza kwenye display networks kuna gharama kubwa kwakuwa unawalipa watu wawili google na mwenye mtandao husika unaoonesha matangazo ya google.

Faida nyingine ya search networks tangazo lako litaoneshwa kwa watu wapya asilimia kubwa kwakua aliyeserch leo google how to make money online hawezi rudia kutafuta kitu kile kile kila siku. Google inaonesha matangazo yako kwa kuangalia mtu anatafuta kitu gani google yaani ameandika maneno gani google  inamletea matangazo yanayoendana na maneneno unayotafuta kwenye google search

Pia unaweza kutangaza biashara kwa bei ndogo mtandaoni hapa jamiihuru.com Bei ndogo kutangaza biashara kuliko mitandao yote duniani sababu jamiihuru.com ni mtanndao unaomilikiwa na watumiaji wote wa mtandao huu. Yaani wamelipia sh elfu 1 kila mmoja kwahiyo gharama za uendeshaji mtandao wamechangia wao sasa kwanini watangaze kwa bei kubwa? Ukitangaza hapa jamiihuru.com unalipia sent chache kwa tangazo likibonyezwa.  Hivyo hapa ndipo sehemu nzuri ya kutangaza blog ili upate wasomai wengi kwenye blog yako, Au tangaza you tube yako upate subscribers 5000 kwa siku. Una app unataka ipate watumiaji wengi hapa ndipo pa kutangaza app wadownload watu zaidi ya elfu 5 kwa siku.

Narudia tena usipoteze pesa kutangaza facebook hutapata matokeo yoyote kwenye biashara yako ya mtandaoni. Kama una maoni au una swali uliza kwenye komenti hapo nitakujibu ipasavyo.

jinsi ya kutangaza biashara mtandaoni

jinsi ya kutangaza biashara instagram

jinsi ya kupata wateja wengi

matangazo ya biashara

 

Natoa ofa pia atakayeanza kutangaza biashara kwa kuweka sh elfu 5 kwenye akaunti yake ya jamiii huru ya kutangazia baishara nitamzawaidia sh elfu 5 bure hivyo atakuwa na sh elfu 10 za kutangazia baishara ndani ya jamiihuru.com