Ongeza kipato kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji


ufugaji wa kuku Aina na banda la kuku wa kienyeji(Elimu ya mwanzo)

Utangulizi

Ufugaji wa kuku wa kienyeji kwenye nchi zinazoendelea hususan Tanzania na Afrika kwa ujumla umekuwa ni wa mazoea. Wafugaji wameshindwa kugeuza mradi huu kuwa biashara na kujiongezea kipato cha kaya zao. Hii imetokana na ukosefu wa elimu ya ufugaji, ukosefu wa mabanda bora, uwepo wa magonjwa mbalimbali kama mdondo na ndui, pia upatikanaji haba wa chanjo za magonjwa.Matokeo yake yamekuwa ni upatikanaji haba wa mazao yatokanayo na kuku.

Mambo ya kuzingatia katika banda.

 

 

* Banda liwe na urefu wa kutosha kumuwezesha mfugaji kuingia ki urahisi na kufanya usafi.

 

 

* Banda lijengwe mahali pasipotuamisha maji au madimbwi ya mbu.

 

 

* Banda liwe na madirisha ya kutosha yanayopitisha mwanga na hewa

 

 

* Weka pumba za mpunga au maranda bandani kiasi cha sentimeta 4-6

 

 

  • Gawa vyumba katika banda lako ambapo kuwe na maeneo ya kutotolea vifaranga na chumba cha majike yanayotaka kuatamia.                                 Aina za kuku wa kienyeji ni.       

* Ching'wekwe(umbo dogo)

 

* Singamagazi ( hupatikana Tabora)

 

* Mbeya

 

* Pemba

 

* Unguja

 

  • Kishingo.   
  • kuchi                                                   Hitimisho

Kuku ndiye mnyama pekee anayeweza kufugwa mahali popote hapa ulimwenguni. Na ufugaji wa kuku ndiyo shughuli inayofanyika kwa wingi duniani kuliko ufugaji mwingine wowote ule. Ewe mjasiriamali kumbuka wingi wa mifugo yako ndio wingi wa kipato chako hivyo kumbuka kanuni hii "start small dream big"

 

692 Views