MAMBO MATANO YA KUZINGATIA UNAPOFANYA JARIBIO (TEST)


Kingi Kigongo ni Mtaalamu wa maswala ya Elimu na Saikolojia.

Mpendwa msomaji wa ULIMWENGU WA ELIMU, ni matumaini yangu kuwa u mzima wa afya njema. Katika makala ya leo nitazungumzia jambo la msingi kabisa unapokuwa unasoma shuleni au chuoni. Jambo hilo ni Jaribio (Test). Jaribio ni kipimo cha kuonesha ni namna gani ulisoma na ukaelewa masomo yako. Hata hivyo unaweza ukawa umesoma na ukaelewa vizuri lakini ukafeli test. Hii inaweza kusababishwa na kupungukiwa na mbinu ambazo ulitakiwa kuzitumia katika test hiyo. Katika makala hii tutaangalia mambo matano ya msingi unayopaswa kuyazingatia unapokuwa unafanya test.

1. Soma maelekezo kwa makini.

Unatakiwa kusoma maelekezo yote kwa umakini mkubwa. Maelekezo hayo yanaweza kuwa ni pamoja na muda wa kufanya test, jinsi unavyotakiwa kujibu, na kadhalika.

2. Soma test yote kwa ujumla

Unatakiwa kusoma maswali yote haraka ili kuokoa muda. Hii itakusaidia kuelewa ni maswali yapi ni magumu pia ni maswali yapi ni rahisi. Maswali yote unayoyaweza unaweza kuyawekea alama.

3. Gawa muda kwa kila swali

Unatakiwa kugawa muda kwa kila swali ili kuepuka kutumia muda mrefu kwenye swali moja na kusababisha kuishiwa na muda.

4. Anza na maswali rahisi unayoyafahamu vizuri.

Baada ya kugawa muda kwa kila swali, anza na maswali rahisi ambayo una uhakika nayo. Baada ya kumaliza maswali rahisi, endelea na maswali magumu.

5. Hakiki majibu yako baada ya kumaliza maswali yote.

Baada ya kumaliza maswali yote, kama muda utakuwepo hakiki majibu yako.

Kama una maoni au maswali usisite kukoment hapa chini. Pia unaweza kuwasiliana nami kwa 0785 711118.

Karibu katika makala ijayo.

330 Views