Hivi ndivyo wajanja wanavyotengeneza pesa mitandao ya kijamii inapofungwa au kuzuiliwa kwa muda

Comments · 210 Views

Vijana wabunifu wafanya biashara ya kutoa huduma ya internet kipindi mitandao ya kijamii ikifungwa.

Kumekuwa na utaratibu wa Mitandao ya kijamii kufungwa au kuzuiliwa katika nchi mbalimbali duniani kama China, Uganda Kenya,Tanzania,guinea na kwingineko kutokana na sababu za kiusalama au kisiasa. Kipindi hiki watu wengi wanakuwa hawawezi kuingia kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, twitter, WhatsApp, Instagram na mitandao mingineyo kama YouTube.

 

Kitendo hiki kinawanyima raha watu wengi waliozuiliwa kupata huduma hiyo kwani so wrote wanatumia mitandao kwa lengo LA kuvuruga amani au kwa malengo ya kisiasa. Wengine mitandao ya kijamii ni kama kilevi, addiction, bila kuingia mitandaoni na kuweka picha, video, au maneno ya kuonesha mtindo wa maisha lifestyle au kutazama wengine wameweka nini watu kama hao wanakuwa wanyonge sana.

 

Fursa inayojitokeza kipindi mitandao ikizuiliwa matumizi

 

Vijana watalaumu wa kutumia app mbali mbali wamejigundulia fursa ya kuunganisha watu na internet kipindi chote mitandao ikiwa imezuiliwa.

 

Wanatumia nini kuunganisha watu au kurejesha huduma ya internet I kwenye simu za mikononi (rununu)

Zipo njia nyingi lakini njia kuu wanayotumia ambayo si rahisi kwa watoa huduma wanaotambulika na serikali hizo kuzuia ni njia ya VPN

 

VPN ni nini?

 

Hii ni app ambayo imebuniwa na watalaumu kwa lengo kuu LA kurejesha huduma za mitandao yote iliyozuiliwa kwenye simu au kompyota.

 

Wanawezaje kudownload app wakati intaneti imefungwa au kuminywa ili isiweze kudownload au kutuma file lolote?

 

Wanatumia prox ambazo zinaficha eneo halisi ambalo mtu yupo. Mfano MTU aliyopo Tanzania anaweza someka yupo uingereza hapo ataweza tumia internet kudownload app hiyo na kuirisha kwenye simu yake au ya mteja na kuunganishwa na internet itakayoruhusu mtu kuingia kwenye mtandao wowote uliozuiliwa au kufungwa.

 

Supper VPN kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini ndio kifaa au app ambayo watu wanatumia kuwarejeshea mtandao watu wengine na kulipwa kiasi kidogo cha pesa.

Mtu yoyote anaweza kutoa huduma hii akiwa tu na simu ya smartphone na file la app ya Supper VPN anaituma kwa Bluetooth file likifika kwenye simu ya mteja anabonyeza na kuinstall kisha kuifungua app ya VPN na kubonyeza connect hapo anakuwa amemaliza huduma za mitandao yote iliyozuiliwa zinarejea kwenye simu ya mteja na mteja anamlipa kiasi cha pesa walichokubaliana.

 

Kwasiku kijana akipata wateja kumi na wakanlipa sh elfu 5 kila mteja anapata elfu 50. Kwa mwezi ana pesa nyingi. Wajasiriamali hawa wanaomba Mungu mitandao iendelee kuzuiliwa ili walate riziki zao.

 

Hii ndio habari ya kiteknolojia ambayo leo utakuwa umeshangazwa nayo au kufurahishwa nayo.

 

 

Follow account yangu like hii post kisha share ili nami nilipwe kwa kupost makala iliyotazamwa na watu wengi asante kwa kushare.

mitandao itafunguliwa lini?

Lini mitandao itafunguliwa?

 

 

Read more
Comments
Search
ADVERTISEMENT
------------------------- Asante kwa kutembelea mtandao huu

Tunaomba msada wako kushare mtandao huu