UFISADI NCHI ZA AFRICA

Comments · 274 Views

Ufisadi ni tabia mbaya ya kuchukua Mali ya umma kwa njia isiyo faa kwa kutumia mamlaka ulionayo.kwa mfano mwanasiasa aliyekatika ngazi za juu serikalini.nchi nyingi hapa Africa viongozi wanatumia mamlaka yao kuvuja Mali ya umma Kama vile naeleza ifuatayo.

Ufisadi ni njia moja mbaya Sana ya kutumia mamlaka kuiba Mali ya umma.Mtu hutumia ushaushi alio nayo ili kuvuja Mali ya umma kujinafsisha na kutajirika nayo.

Ufusadi umekitiri Sana katika viongozi haswa wa kiafrica, wale wako viongozini wanatumia mbinu kadhaa kufuja Mali ya umma kujinafsisha na kutajirika.Wanafanya hivo bila kujali shida wanazo pitia wanchi wa kawaida.wananchi wengine haswa wa kiafrica wanakosa raslimali muhimu kwa maana viongozi hubokonya kila raslimali inayo faa mwananchi wa kawaida.

Nchi kadha katika utapata matajiri ni wachache haswaa walio na vyeo na wengi ni maskini na maskini atazidi tu kuwa maskini.

Ufisadi umeenea Sana haswa nchi yangu ya Kenya.kila kiangozi ni mfisadi kuanzia juu Hadi chini.maisha yamekuwa magumu Sana kwa maana hawa viongozi waharibu uchumi wa nchi kwa ajili ya manufaa yao.

Kila kitengo Cha serikali umeejaa ufisadi.kuanzia mawaziri Hadi mabunge ya Jimbo alafu wanaongoza na magavana wa majimbo.swali ni he?ni lini ufisadi utaisha na mbinu gani zitatumika kumaliza ufisadi?

Inafaa sisi kama wananchi tuwe waangalifu Sana tunapo chagua viongozi haswa wa kisiasa na kuimarisha democrasia za nchi zetu.

Umaski umekitiri kila uchao akuna maji,akuna chakula ,akuna Karo za shule,akuna ajira ukitaka ajira lazima hongo, biashara haipo jamani tutaendeleza maisha vipi na ufisadi.

Tunawakumbusha vitengo vya kiserikali huru wanaohusika na ukabidhiliaji wa ufisadi wakaze kamba ili wamalize ufisadi nchini kwa maana hauna manufaa yoyote kwa wananchi.

Tunaomba vijana,wazee ,wamama na viongozi wa kidini tujitokezee na kukataa ufisadi.Yafaa tupinge ufisadi kwa njia yote inayo stahili na kuomba mungu awakanye viongozi visadi.Ufisadi unaendeleza umaskini kwa wanchi wenye mapato madogo na wao ndio wako wengi Sasa ya faa kufanya maamuzi wenye busara kwa kuchagua viongozi kakamavu na wasio na ufisadi.Tuungane pamoja kwa Hali na Mali ili tuangamize ufisadi Africa na ulimwengu kwa ujumula ili tupunguze umaskini ambao umekita mizizi.Najua umoja ni nguvu utangamano ni udhaifu kwa hakika tukiungana tutamaliza ufisadi.Asante Mimi ni mzaliwa wa Kenya # zakayo kemboi

Read more
Comments
Search
ADVERTISEMENT
------------------------- Asante kwa kutembelea mtandao huu

Tunaomba msada wako kushare mtandao huu