JIFUNZE KILIMO

Comments · 101 Views

JIFUNZE FAIDA NA HASARA ZA KUFANYA KILIMO.

kilimo ni nini?

kilimo ni uzalishaji wa mazao kwenye mashamba.mtu anayejishughulisha na kilimo huitwa MKULIMA.

 kwa maana pana inajumuisha mifumo ya uzalishaji mimea,ufugaji wa wanyama na uvuvi wa samaki.mara nyingi ufugaji wa wanyama huendana na kilimo cha mimea.

FAIDA ZA KILIMO

1.kuboresha ajira katika uzalishaji wa kilimo.

2.kuzuia hasara za udongo.

3.kudumisha ubora wa maji.

4.huongeza mapato ya wazalishaji

5.inahifadhi nishati.

HASARA ZA KILIMO

1.Kupata mavuno kidogo.

2.kukosekana kwa soko.

3.ubora hafifu wa mazao.

kwa kifupi ni kwamba kilimo kina faida nyingi mno kuliko hasara zake,cha msingi katlka kilimo ni kufanya shughuli hii kwa malengo na mipangilio,ili uweze kuona faida yake ipo wapi.kumna namna  mbalimbali za kuweza kufanya kilimo kwa mfano;unaweza fanya kilimo cha mbogamboga ambacho chenyewe kinahitaji mtaji mdogo sana kukifanya ingawa faida yake ni kubwa.kilimo cha viungo,hapa namaanisha nyanya,kitunguu maji,kitunguu swaumu,karoti,pilipili hoho,pilipili za kawaida nk.

MIFANO YA MBALIMBALI YA KILIMO

kilimo cha NYANYA

mara nyingi hutumika kama kiungo cha mboga,vilevile nyanya hulimwa sehemu nyingi sana duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kama zao la biashara.

kwa hapa Tanzania zao la nyanya hulimwa zaidi kuliko mazao mengine ya mbogamboga.kuna mambo mawili ya kuzingatia katika kilimo cha nyanya;

-hali ya hewa.

katika hali ya hewa inatakiwa mkulima azingatie kulima nyanya zake katika mazingira ya joto la wastani na vilevile asije lima nyanya katika mazingira ya mvua nyingi maana mvua nyingi husababisha magonjwa katika kilimo hiki.

-udongo

katika udongo mkulima anatakiwa ahakikishe eneo anlolima lina mbolea ya kutoshana ni eneo lisilosimamisha maji,vilevile katika kichanga,mfinyazi mkulima anaweza kulima nyanya.

kuna AINA kuu mbili za nyanya

1.nyanya ndefu

2.nyanya fupi

FAIDA ZA KILIMO CHA NYANYA

zao hili la nyanya lina faida sana kiukweli na vijana wengi sasa hivi wanalima zao hili kwani sio gumu kivile kama ukifuata taratibu zake za ulimaji kuanzia kusafisha shamba ,kuwatika mbegu na hadi kuapandikiza miche yake kwenye matuta uliyoyaanda.lakini usipofuata taratibu zake utachukia kilimo hiki na kuona mimi ninaekueleza ni muongo kabisa,lakini kiukweli watu wanasomesha na kuendesha maisha yao mengine kwa kufanya kilimo cha nyanya.

huongeza kipato

walio wengi hufanya kilimo kama njia yao ya kujiingizia kipato,yaani hishi na kuendeleza maisha yao kwa kupitia kilimo hiki cha nyanya.

kukuza uchumi

hapa katika uchumi ni hasa kwa serikali,uchumi wa nchi unakuwa kutoka na kodi zinazopatikana kutokana na mauzo ya zao la nyanya hasa linapouzwa kwenda nchi za nje.

kulinda na kutunza ardhi.

vilevile kilimo cha nyanya ni njia moja wapo ya kutunza rutuba ya shamba lako na kutunza ardhi kutoka kwa wanyang'anyi.pale shamba linapoonekana linafanyiwa kazi ni vigumu hata watu kulivamia yaani linakuwa salama salimini kutokana na kilimo cha nyanya.

HASARA ZA KILIMO CHA NYANYA

kushuka kwa bei

hapa kuna muda zao la nyanya hushuka bei sana sokoni kutokana na uvunaji wake unakuwa ni kwa wingi sana.lakini hili lisisikupe changamoto kwamba usifanye kilimo cha nyanya kwani sio kila mara bei ya nyanya hushuka.

kupata mazao kidogo

nyanya ni moja ya zao ambalo katika uvunaji wake unaweza ukapata mazao kidogo tofauti na ulivyotegemmea.lakini hasa hutokana na wewe mwenye taratibu ulizozifuata katika ulimaji wako kuanzia uandaaji hadi kuvuna.sababu ya mazingira pia huchangia nyanya kuwa hafifu na mkulima kupata mazao kidogo(hali ya hewa).

Comments