Mikopo kwa wafanyakazi soma hapa kabla hujapata shida

Comments · 169 Views

Kama wewe umeajiriwa hivi karibuni soma hapa kisha watumie na wenzio whatsapp, twitter na Facebook

Mikopo ya wafanyakazi soma hapa kabla hujapatashida


mikopo ya haraka bila dhamana
mikopo ya crdb kwa wafanyakazi
mikopo kwa njia ya simu
riba ya mikopo crdb 2021
mikopo ya nmb kwa wajasiriamali
mikopo ya nmb na riba zake
mikopo binafsi nssf
mkopo kwa dhamana ya kiwanja

Watu wengi wamekuwa wakitamani kuwa na maisha mazuri. Hata wewe ndugu msomaji wa makala hii unatamani upate maisha mazuri na maisha mazuri ni pesa. Ukitaka elimu nzuri lazima utumie pesa, ukitaka matibabu bora lazima uwe na pesa, Kwa wanaume wakitaka mke mzuri lazima wawe na pesa unaweza biasha lakini ukweli utabaki kuwa ukweli.

 Mikopo Ya CRDB Bank Kwa Wafanyakazi (CRDB Bank Loans To Employees) » All  Global Updates

Mfanyakazi wa serikali au sekta binafsi anapogundua kuwa mshahara wake hautoshi kutatua matatizo au kuanzisha biashara kubwa anayotamani suruhisho ni kuanza kutafuta taasisi za mikopo kama brac, CRDB, NMB Bayport na taasisi nyingine unazozijua. Je yupo sahihi au ndo anajitafutia matatizo zaidi? majibu yote yapo hapa www.jamiihuru.com

Kama unataka mkopo kwa ajiri ya kutatua shida fulani mfano umeajiriwa hivi karibuni sasa huna pesa ya kujikimu na mshahara haujaanza kutoka basi kopa lakini kopa kwenye taasisi za mikopo ambazo riba yake ni ndogo zaidi ukilinganisha na Taasisi zote.

Usidanganyike na taasisi za mikopo ya haraka ambayo wewe unazani ipo kwa ajili ya kukusaidia haraka kutatua shida zako kumbe zipo kukuharibia maisha zaidi kwa kukutoza riba kubwa ambayo itazaa matatizo makubwa mbele na utaendelea kuwa mteja wao maishani hatimaye mshahara wako utakuwa unagawana nao miaka yote kama vile walikosomesha wao.

Usichukue  mkopo kwa ajiri ya kuanzisha biashara mpya pindi tu unapoajiriwa narudia tena usichukue mkopo kwa kudhani unaweza fanya biashara itakayokupa faida kubwa ili riba ikatwe kwenye mshahara wako kidogo kidogo. Nimerudia mara mbili nikimaanisha na ukijifanya hujaelewa ukakopa basi baada ya mwaka mmoja utakuja kutoa ushuhuda hapa jinsi mkopo uliochukua unavyokutesa na hujui utatuaje shida hiyo.

Watumishi hasa wa serikalini wakiajiriwa tu haipiti miezi minne wanaanza kukopa kwa ajili ya kuanzisha biashara baada ya hapo kinachofuata biashara zinafeli kama ilivyo kawaida kwa biashara yoyote kufeli. Sasa amekopa milioni 5 mfano marejesho milioni 8 hapo anatakiwa atafute milioni 3 za kuilipa taasisi aliyokopa mfano Platnum credit kinachofuata ni kwamba hizo milioni 8 zitakatwa taratibu kwenye mshahara wake mpaka ziishe sasa kwa mfano kila mwezi wakakata 150,000 je deni litaisha baada ya miaka mingapi?

Hapo kwenye mshahara wako kuna makato ya lazima kama bodi ya mikopo ya elimu ya juu kama ulisoma chuo kwa kufadhiliwa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu HSLB. bado makato ya pesheni PSPF bado kodi ya taifa, Bado bima ya afya yaani kama ulikuwa unapokea laki 7 unajikuta sasa unabaki na 200,000 ndo mshahara wako kumbuka maisha ya sasa wastani wa pesa ya kukuwezesha kuishi kwa siku kwa mfanyakazi wa serikali  ni elfu 10 mwezi una siku 30 wewe una laki mbili kamili ambazo ukianza kuzitumia tarehe moja kufika tarehe 20 laki mbili imeisha bado siku 10 ili upate mshahara mwingine hapo kitakachofuata ni stress kama wewe ni mwalimu utajikuta fimbo kwa wanafunzi zinaongezeka hasira hasira haziishi, familia nayo unaichukia watoto ni kuwafokea bila sababu hapo ujue mchawi wako sio hao unaowakasirikia mchawi wako ni ile taasisi iliyokushawishi ukope.

Hii ndio jamiihuru.com tunapeana elimu ya kweli ya maisha sio udaku usio na tija

Read more
Comments
Search
ADVERTISEMENT
------------------------- Asante kwa kutembelea mtandao huu

Tunaomba msada wako kushare mtandao huu