Serikali kufunga mitandao ya kigeni facebook, instagram, twitter na mingineyo:Ushauri

Comments · 10 Views

Tanzania ina uwezo wa kuifunga mitandao ya kigeni kama facebook twitter instagram whatsapp facebook na mingineyo

Serikali kufunga mitandao ya kigeni facebook, instagram, twitter na mingineyo Ni ushauri tu

aina za mitandao ya kijamii
mitandao ya kijamii tanzania
faida za mitandao ya kijamii
mitandao ya kijamii in english
tcra

Kumekuwa na mitandao mingi sana ya kigeni kama facebook twiter instagram whatsapp na mingineyo ambayo watanzania wanaitumia sana kuchat na kutangaza biadhaa zao, Mitandao hiyo inachuma pesa nyingi sana toka Tanzania kwakua watumiaji wa mitandao hiyo wanatangaza biashara zao na kuyalipa makampuni yanayo toa huduma hizo ambazo zinaweza kutolewa na watanzania wazalendo mfano mtandao wa www.jamiihuru.com ni kama facebook na unamilikiwa na Mtanzania.

Kuna sheria ya mitandao iliyotungwa mwaka 2015 Tanania ikiwataka wamiliki wa mitandao kama blog youtube channel kulipia tozo za leseni a kuweka maudhui sheria hiyo kwa mtazamo wangu naona ilifunga mitandao mingi iliyomilikiwa na watanzania hivyo mitandao ya kigeni ilipata umaarufu zaidi kwakua watu hawawezi kupata mitandao ya kizalendo ili waweze kuwasiliana na kutangaza biashara zao au huduma wanaamua kwenda facebook twitter instagram kuchat na kutangaza biashara zao matokeo yake pesa ya tanzania anaichuma mmiliki wa facebook instagram google na mitandao mingine na mmiliki huyo sina uhakika hata kama analipa kodi kwa watanzania hawa ambao anavuna pesa zake.

Ushauri ni kwamba Tazania ifunge mitandao ya kigeni yote na kutengeneza fursa kwa watanzani kumiliki mitandao kama hii ya www.jamiihuru.com au  blogs App za kuchat kama whatsapp telegram watanzania tunauwezo wa kuzimiliki. Hapo pesa yetu ya Tanzania haitatoka kwenda nje kwakua tutatangaza baishara zetu kwenye mitandao ya Tanzania kama huu wa www.jamiihuru.com na pia wamiliki wa mitandao hiyo watalipa kodi kwa serikali kwaku watakuwa wanapata kipato kizuri.

Mfano mimi nimeshatangaza biashara facebook nikilenga wateja wa Tanzania nimetumia zaidi ya dola 500 sawa na milioni na zaidi kwa pesa ya Tanzania na pesa hizo zipo marekani kwa sasa zinajenga uchumi wa marekani kwa bahati mbaya hata faida ya kutangaza sikuipata kwakua ukitangaza facebook tangazo lile lile linaweza kuoneshwa hata mara mia moja kwa mtu mmoja na utalipia pesa kama vile wametazama watu mia moja tofauti. Lakini kama kungekuwa na mitandao ya kizalendo ningetangaza biashara zangu kwenye mitandao ya Tanzania na pesa ingebaki kwa watanzania wenzangu

 

Sijaona faida yoyote kubwa ya kutegemea mitandao ya kigeni hapa Tanzania lakini naona tu hasara nyingi kama kuchangia mmmonyoko wa maadili yetu kutoa pesa zetu kwenda nje ya nchi badala ya kupata pesa za kigeni, kudhoofisha usalama n.k  Unaweza kuchangia hoja hii jinsi unavyofikiria comment hapo chini. Kwanini Tanzania isiifungie mitandao yote ya kigeni isitoe huduma Tanzania au walipe kodi tena kubwa ili Tanzania yetu iweze kunufaika zaidi Karibu

Read more
Comments
Search
ADVERTISEMENT
------------------------- Asante kwa kutembelea mtandao huu

Tunaomba msada wako kushare mtandao huu