SHETANI YUMO MAKSNISANI
Siku moja nikiwa nikiwa ibadani kama mwongozaji mkuu wa ibada, aliletwa binti mmoja mwenye mapepo wachafu akiwa amebebwa na watu sita.
Wakamleta hadiadhabahuni, na kumbe alikuwa ni kiongozi wa sifa hapo Kanisani; lakini alikuwa amepagawa na mapepo.
Nikasema mkono juu yake ili kumwombea, nilipoweka tu mkono wangu kichwani pake nguvu zangu za kiroho zilikata. Mbingu zikafungwa. Binti akawa anacheka sana kwa nguvu za yule pepo. Akaja Mchungaji mkuu, tukamwombea kwa pamoja lakini pepo hakutoka, bali alicheka sana kwa dharau huku akimwangalia mchungaji.
Mchungaji akasema tumwache;
roho yangu iliniuma sana, nikaingia chumba cha ofisi cha kanisa, Nikakulia kwa uchungu mbele za Mungu. Nikimwuliza Mungu tatizo ni nini? Na sababu ni nini ya jambo hili la aibu? Nikiwa naendelea kumlilia Mungu, ndipo kwa maono nikamwona yule binti kuanzia paji lake la uso kuja mbele ni yeye, lakini kurudi mgongoni ni joka kubwa sana lenye mkia mrefu lenye magamba makubwa mgongoni yaliyosimama kama panga za samaki aina ya Papa.
Ajabu ni kwamba sikuogopa.
Nikamwukiza Mungu" kwani maombi tunayofanya ya kuweka ulinzi kwenye Malango, Mipaka na kila Njia juu ya mahali hapa, Bwana huwa hujibu?
Bwana akanijibu, unakumbuka kuwa nyoka hakufukuzwa katika bustani ya Edeni? Na je, imeandikwa nini katika Ayubu sura ya kwanza"? Nilipokumbuka hayo, uchungu wangu uliisha na maombi yangu yakakata.
Ninatoka nikiwa mwenye amani.
Kesho binti akaja Kanisani kwa ajili ya kuimba, nikamwita pembeni, nikamwambia, niambie wewe ni nani na asili yako pia, hapo nilimwuliza nikiwa nimejaa nguvu za Mungu. Macho ya binti yakawa mekundu na madogo na akawa na hasira, hakujibu kitu ila alitaka kufanya kitu kwangu lakini alishindwa. Akaondoka kwa hasira na hakurudi tena Kanisani na akahama kabisa kijijini hapo.
Nikaja kusikia kwa rafiki yake wa karibu kwamba ameandika kwa sababu mimi nimemjua kuwa yeye ni nani.
Imeandikwa:
Kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi.
Enyi waombaji, Vunjeni kazi za ibilisi makanisani ili watu wapokee Miujiza yao. Ni kwa Neno na Maombi tu, Mungu anatenda kwa ukubwa.
Amen. Barikiweni sana.